Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
VIONGOZI WA HALMASHAURI YA MBULU WAPATIWA ELIMU YA HUDUMA ZA COASCO SABASABA 2026
19 Jul, 2026
VIONGOZI WA HALMASHAURI YA MBULU WAPATIWA ELIMU YA HUDUMA ZA COASCO SABASABA 2026

VIONGOZI WA HALMASHAURI YA MBULU WAPATIWA ELIMU YA HUDUMA ZA COASCO SABASABA 2026

Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Dkt. Emmanuel Qambaji Nuwas, akiambatana na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, leo Julai 6, 2026, wametembelea banda la Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026).

Katika ziara hiyo, viongozi hao walipata elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na COASCO, ikiwemo ukaguzi wa hesabu za vyama vya ushirika na Taasisi nyingine, ushauri wa kitaalamu, mafunzo na huduma za usimamizi wa vihatarishi, zinazolenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na utawala bora katika sekta ya ushirika