Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
TRA YAITAMBUA COASCO KWA UZINGATIAJI BORA WA SHERIA NA TARATIBU ZA KODI
26 Sep, 2026
TRA YAITAMBUA COASCO KWA UZINGATIAJI BORA WA SHERIA NA TARATIBU ZA KODI

TRA YAITAMBUA COASCO KWA UZINGATIAJI BORA WA SHERIA NA TARATIBU ZA KODI

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limetambuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kiwango kizuri cha uzingatiaji wa sheria, kanuni na miongozo ya kodi katika utekelezaji wa majukumu yake kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Akizungumza katika hafla hiyo Septemba 24, 2026 jijini Dodoma, Naibu Kamishna wa Operesheni, Idara ya Walipakodi Wakubwa, Eva Raphael, amesema utambuzi huo unalenga kuthamini taasisi zilizoonesha kiwango kizuri cha uzingatiaji wa sheria na taratibu za kodi, huku akizihimiza kuendelea kudumisha uzingatiaji huo

COASCO imeeleza kuwa itaendelea kuimarisha mifumo ya ndani na kuhakikisha shughuli zake zinafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya kodi, ikiwa ni sehemu ya kujenga taasisi yenye uwajibikaji na uadilifu